Maguri aanza kazi Oman


Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Stand united ya Shinyanga Elias ameanza kazi yake rasmi baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi uko Oman.

Maguri kwa sasa anakipiga katika timu Dhofar FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza ambapo jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Al Etihad.

Dhofar ilishinda 2-1 huku mtanzania Elias Maguri akiongoza safari hiyo ya ushindi wa Dhofar FC.

Maguri ana kazi nzito kutengeneza jina lake na kuinyanyua timu hiyo iweze kupanda daraja na kushiriki ligi kuu.

Comments