Man city yapeleka jina la Stones UEFA.


Beki Everton John Stones huenda akatua Manchester city muda wowote kuanzia sasa baada ya jina lake kujumuishwa UEFA.

Manchester city imetuma kikosi cha wachezaji watakaocheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na Stones akiwemo.

Makubaliano ya usajili wa mchezaji huyo baina ya Everton na Manchester yanaendelea vizuri dili hilo litakamilika muda wowote kuanzia sasa.

Stones amekuwa akitolewa macho na timu mbali mbali lakini City wanaonekana kuwapiku vigogo wengine barani Ulaya katika mpango wa kumsajili beki huyo wa England.

Comments