Man united yanyanyua ngao ya hisani


Timu ya Manchester united leo ikiwa Wembley imefanikiwa kunyakua ngao ya hisani baada ya kuilaza Leicester city kwa bao 2-1.

Man united ilipata bao la kuongoza kupitia Jesse Lingard, lakini Jamie Vardy alichomoa bao hilo kipindi cha pili.

Hata hivyo Zlatan Ibrahimovic aliipatia Man united bao la pili na la ushindi baada ya kuunganisha krosi safi ya Antonio Valencia.

Comments