Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake ya uenyekiti na ufadhili katika timu hiyo.
Hatua hiyo imekuja kutokana na Kashfa zinazosadikika kufanywa na baadhi ya wanachama wa Yanga ambao hataki mwenyekiti akabiziwe klabu hiyo.
"Najiuzulu rasmi katika nafasi ya uenyekiti, hii ni klabu yangu, pia naifadhili kwa pesa yangu, kuna maneno si mazuri kwa baadhi wanachama ambao hawapendi uwepo wangu."
"Najiuzulu hayo ndiyo maamuzi yangu." Alisema Manji
Mwenyekiti huyo amekuwa akilalamikia kuwepo kwa wanachama ambao wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya viongoz wakubwa kuichafua nafasi yake.

Comments
Post a Comment