Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji leo hii ameongoza wanachama na mashabiki wa Yanga kuuaga mwili wa Baba wa mchezaji Deogratius Munishi “Dida.” Mzee Munishi aliyefariki siku ya Jumapili anasafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Wengine walioaga mwili wa mzee Munishi ni Makamu wa rais wa Simba Geoffrey Nyange Kaburu pamoja na wachezaji mbalimbali, shughuli iliyofanyika katika kanisa katoliki Chang’ombe.
Mchezaji huyo alipokea taarifa ya kufiwa na Baba yake mzazi baada ya mchezo wa timu yake dhidi ya Afrika Lyon mechi ambayo Yanga ilishinda jumla ya goli 3-0, huku kipa huyo akiwa langoni.
Comments
Post a Comment