Mbeya city yavutwa shati na Kagera Sugar


Timu ya Mbeya city leo ikiwa ugenini imeshindwa kutamba mbele ya Kagera Sugar baada ya kutoka sare isiyokuwa na magoli.

Timu zote zilionekana kuwa na umakini hasa kwenye safu ya ulinzi ambayo kwa upande wa timu zote ilionekana kuwa imara.

Kwa upande wa Kocha wa Kagera Mecky Mexime alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri na timu yake itazidi kuimarika.

"Tumecheza vizuri na pia ligi ndiyo inaanza nadhani tutazidi kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda." Alisema Mexime

Pia kwa upande wa kocha wa Mbeya City Kina phiri ameisifu safu yake ya ulinzi huku akisisitiza kuwa ataendelea kuimarisha safu ya ushambuliaji.

"Safu yangu ya ulinzi ilikuwa imara sana lakini bado kuna mapungufu madogo kwenye safu ya ushambuliaji, hilo nitalifanyia kazi." Alisema Phiri.

Comments