Messi arejea timu ya taifa


Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi amekubali kurudi na kuendelea kuitumikia timu ya taifa.

Baada ya Argentina kuchemsha kwenye michuano ya Copa America Juni mwaka huu mchezaji huyo aliamua kustaafu soka la kimataifa.

Hata hivyo serikali ya Argentina iliamua kuingilia kati suala hilo na kumuomba Messi abadilishe maamuzi yake na kurejea kwenye timu hiyo.

"Niliamua kustaafu ili nisiliumize tena taifa langu na nami nisiumize moyo wangu, lakini nchi yangu inanipenda, nami naipenda hivyo nimeamua kurejea tena." Alisema Messi

Mchezaji ataanza kuitumikia timu hiyo hivi karibu katika mechi za makundi kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Urusi mwaka 2018.

Comments