MO amwanga milioni 100 za usajili Simba

MO akimkabidhi hundi ya milioni 100 raisi wa Simba

Mapinduzi na mabadiliko ndani ya Simba yameanza kunukia baada ya Mohamed Dewji maarufu kama MO kumkabidhi hundi ya milioni 100 Raisi wa Simba Evans Aveva.

MO alikabidhi mfano wa hundi hiyo akiwa ofisini kwake katika jengo la Jubilee Tower mtaa wa Ohio Dar es Salaam.

Raisi wa Simba Evans Aveva alitoa shukrani za dhati kwa Mohamedi Dewji kwa Mchango huo wa shilingi milioni 100 huku akiongeza kuwa bado wanahitaji milioni 320 ishirini za usajili.

Mfano wa hundi aliyokabidhi kwa raisi wa Simba

"Ninashukuru kwa msaada kutoka kwa mwanachama wetu, na sasa tutaweza kukamilisha usajili wa Fredrick Blagnon kutoka Ivory Coast." Alisema Aveva.

MO alihaidi kuichangia Simba kiasi cha fedha kwa ujali ya usajili na leo mmiliki wa kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) ametimiza ahadi yake.

Comments