Uongozi wa timu ya Simba umekubali klabu hiyo kuendeshwa kwa mfumo wa hisa baada ya makubaliano baina ya kamati tendaji ya Simba na Mohamed Dewji.
Nakala iliyotolewa na afisa habari wa timu ya Simba Haji Manara kwa waandishi wa habari imethibitisha kuanza rasmi kutumika kwa mfumo huo ndani ya timu hiyo.
MO ambaye ni mkurugeni wa kampuni ya METL katika mkutano uliofanyika Julai 31 mwaka huu alieza kwa wanachama na wajumbe wa Simba mifumo mbalimbali ambayo itatumika kuendesha hisa hizo.
Watekelezaji wakuu wa mfumo huo ambao ni kamati ya utendaji Simba wameridhia mabadiliko hayo na sasa kilichobaki ni utekelezaji wa zoezi hilo.

Comments
Post a Comment