Mtanzania ashika namba tano Mkenya akiwa Bingwa

Mwanariadha wa Kenya Eliude Kipchoge ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon kilometa 40 katika siku ya mwisho ya mashindano ya Olympiki jijini Rio nchini Brazil.

Mkenya huyo alitumia muda wa saa 2 na dakika 8 na sekunde 44 na hivyo kunyakuwa medali ya dhahabu, huku Muethiopia akishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikichukuliwa na raia wa Marekani.

Katika mbio hizo zilizowashirikisha Watanzania watatu, Alphonce Felix Simbu alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 11 na sekunde 15 amemaliza katika nafasi ya tano.

Watanzania wengine ni Said Juma Makula aliyeshika nafasi ya 43 akitumia muda wa saa 2, dakika 17 na sekunde 49 huku Fabian Joseph akishika nafasi ya 112 akitumia muda wa saa 2, dakika 28 na sekunde 31.
Mbio hizo zilishirikisha wanariadha 155 wakiwakilisha mataifa 80

Comments