Mustafi
Nyota wanaowindwa na Arsenal kwa muda sasa Shkodran Mustafi pamoja Lucas Perez watatua London ili kufanyiwa vipimo.
Wenger amefikia makubaliano ya makubaliano ya ada Uhamisho wa £35 milioni kwa Shkodran Mustafi ambaye ni beki wa Valencia pamoja na kiasi cha £17 milioni kwa strika wa Deportivo Lucas Perez.
Timu ya Arsenal ina mapungufu kwenye safu ulinzi, kutokana na baadhi ya wachezaji kukumbwa na majeraha akiwemo Per Martasacker ambaye atakaa nje uwanja kwa muda mrefu.
Pia Arsenal ina mapungufu kwenye safu ya ushambuliaji na Wenger ameamua kulikabili tatizo kwa kumsajili Lucas Perez aliyefunga goli 17 msimu uliopita katika ligi ya Hispania.
Perez
Arsenal ilianza kumfuatilia Lucas Perez kwa muda mrefu na sasa Wenger amejiridhisha kumsajili mshambuliaji huyo wa Hispania.


Comments
Post a Comment