Mzee akilimali abebeshwa mzigo wa lawama Yanga


Wengi wa mashabiki na baadhi ya wanachama wa Yanga wamemlaum mzee Ibrahim Omary Akilimali kuwa chanzo cha kujitoa kwa Yusuph Manji.

Wanachama na viongoz wa matawi mbalimbali wamemtuhumu mzee Akilimali kuwa ndiye aliyechangia mwenyekiti huyo kujitoa katika udhamini wa timu hiyo.

Mapema leo Mzee Akilimali aliwasili kwa kwenye jengo la ofisi ya timu hiyo maeneo ya Jangwani kuwataka radhi wanachama na mashabiki.

Hata hivyo wanachama na viongozi wa matawi mbalimbali wameutaka uongozi kumsimamisha uanachama mzee huyo kutokana na kauli zake tata ambazo zimechangia Yusuph Manji kuchukua uamuzi huo.

Comments