Nape atoa baraka zake Simba


Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametoa baraka zake kuitakia kila la heri Simba katika mpango wake wa kuikabidhi timu kwa mohamed Dewji.

Mh. Nape katika ukurasa wake wa twitter aliandika kuwa endapo mfumo huo utasimamiwa vizuri na timu hiyo utakuwa na tija.

Siku chache zilizopita mmiliki wa kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited 'MO' aliweka wazi mpango wake wa kununua 51% ya kununua hisa za timu kwa thaman ya bilioni 20 za kitanzania.

Licha ya viongozi wa Simba kuonekana kusita kupitisha mpango huo kwa haraka lakini msimamo wa wanachama na wapenzi wa Simba ni kuona MO anakabidhiwa timu hiyo.

Comments