Negredo amerudi vizuri EPL


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester city ambaye kwa sasa anakipiga Middlesbrough amerudi vizuri  England baada ya kutupia bao la kuongoza dhidi ya Stoke.

Negredo 30, ameingia kwenye orodha ya wafungaji ikiwa leo ni siku ya kwanza msimu mpya wa ligi umefunguliwa.

Mbali na Middlesbrough ya sasa Negredo alikuwa mtupiaji mzuri wa magoli akiwa na Sergio Aguero ambao kwa pamoja waliongoza jahazi la city kuchukua ubingwa wa ligi msimu wa 2013/14.

Comments