Timu ya Newcastle chini ya kocha yake Rafael Benitez walianza vibaya baada ya kuchezea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Fulham.
Fulham iliwakaribisha Newcastle katika uwanja wa Craven Cottage ambapo ndani ya kipindi cha kwanza timu ilipata bao la kuongoza kupitia Matt Smith aliyefunga kunako dakika 45 ya mchezo.
Hata hivyo Fulham walimiliki zaidi mchezo na kuyafanya matokeo kubaki 1-0 hadi mwisho wa mechi hiyo.
Pamoja na kuanza vibaya kwenye ligi hiyo bado Newcastle ipo kwenye kibarua kizito cha kuzuia baadhi ya nyota wake wasiondoke kwenye timu akiwemo Mousa Sissoko.

Comments
Post a Comment