Ngoma afunguka jinsi anavyoinjoi Yanga


Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma amesema ana furaha na timu yake sasa tangu alipojiunga akitokea Platinum ya Zimbabwe.

Ngoma alifunguka hayo katika mahojiano na Cafonline.com ambapo alithibisha kuna ushindani zaidi katika timu ya Yanga kuliko Platinum.

"Tangu nilipojiunga na Yanga kuna tofauti ya ushindani na nilipokuwa, nafurahia maisha ya hapa na jambo kubwa ni kutimiza wajibu wangu ikiwemo kufunga magoli." Alisema Ngoma

Ngoma aliongeza kuwa uwepo wa Thabani Kamusoko kwenye timu hiyo unazidi kumpa mafanikio kwa kuwa wamecheza soka pamoja kwa muda mrefu.

"Uwepo wa Kamusoko unanifanya nicheze soka vizuri, nimecheza naye kwa muda mrefu Platinuma nadhani kuna vitu tunafanya uwanjani si vigeni kwetu kwa kuwa tuna maelewano ya muda mrefu uwanjani." Alisema mchezaji huyo

Ngoma ameifungia Yanga jumla ya mabao 3 kwenye michuano ya kombe la shirikisho, akiwa kinara wa mabao kwenye timu hiyo.

Comments