Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma ataikosa mechi ya Marudiano dhidi ya MO Bejaia ya Algeria kutokana na idadi ya kadi mbili za njano.
Yanga itashuka dimbani Agosti 13 mwaka huu kwenye kwenye mchezo wa tano katika kundi A bila Ngoma ambaye ni sheria kutumikia adhabu hiyo.
Ngoma mwenye magoli manne kwenye michuano hiyo amekuwa nguzo imara siku zote katika kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu ya Yanga na kutikisa ngome pinzani.
Yanga ina kibarua cha kutafuta ushindi kwa hali na mali kutokana na kuambulia pointi moja pekee hadi sasa baada ya kupoteza michezo mitatu ili kurejesha matumaini yake kusonga mbele.

Comments
Post a Comment