Ni Arsenal v Liverpool usikose game hii


Arsenal katika uwanja wa Emirates leo itaikaribisha Liverpool ikiwa ni mechi yao kwanza ya ufunguzi kwenye ligi.

Msimu uliopita Arsenal na Liverpool zilipata matokeo ya sare katika mechi zote mbili walizokutana na kugawana idadi ya pointi 1.

Macho ya wengi leo ni kuona nani atakuwa na mbinu za ushindi katika ya Arsene Wenger ambaye ni mwalimu wa Arsenal na Jurgen Klopp kwa upande wa Liverpool na kujihakikishia pointi 3.

Mechi hii inacheza leo majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja emirates, jijini London.

Comments