Leo katika uwanja wa taifa kutatimka vumbi kati ya Yanga na Azam katika mchezo wa ngao ya hisani.
Mechi hiyo huchezwa siku chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi, ambapo aina hii ya mechi huchezwa kwenye ligi nyingi duniani.
Azam ina kumbukumbu ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga katika mechi ya mwisho waliyokutana kwenye fainali ya kombe la shirikisho.
Ngao ya hisani huchezwa kwa ajili ya kusapoti makundi yasiyojiweza kwenye jamii ikiwemo maskini, wagonjwa, walemavu au yatima.

Comments
Post a Comment