Kocha wa Simba Joseph Omog amesema kuwa Simba itaendelea na moto ulel ule wa ushindi dhidi ya Maafande JKT Ruvu leo katika uwanja wa taifa.
Simba ilitoka kifua mbele wiki iliyopita baada ya kuichapa Ndanda bao 3-1 na kuzidi kujenga imani yao kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo.
"Malengo yetu ni kupata ubingwa msimu huu, tulianza na ushindi, pia tutaendelea na ushindi, tumejipanga na tuko vizuri." Alisema Omog.
"Kila timu imefanya maandalizi, kwa upande wetu tumejiandaa kwa ajili ya kuondoka na pointi 3." Aliongeza Omog
Pia Yanga ambayo ilikosa mechi ya ligi wiki iliyopita, kesho itashuka dimbani dhidi ya JKT Ruvu.

Comments
Post a Comment