Palace yakubali £32 M kwa Benteke


Timu ya Crystal Palace imekubali dau la £32 milioni iliyowekwa na Liverpool kama ada ya uhamisho wa mshambuliaji Christian Benteke.

Awali Liverpool ilikataa ofa ya £27 milioni iliyowekwa na Palace siku chache zilizopita na kuitaka Palace ifikie dau la sasa.

Liverpool ilimnunua Benteke mwaka mmoja uliopita kwa £32.5 milioni na licha ya kwamba strika huyo si chaguo la Jurgen Klopp lakini Liverpool imeamua kumuuza kwa gharama ile ile.

Palace ambayo imewauza Dwight Gayle kwenda Newcastle na Yannick Bolasie Everton imeamua kuweka rekodi ya usajili kwenye timu yao ili kuziba mapengo ya wachezaji wao kwa kumnasa Benteke.

Muda wowote kuanzia sasa mchezaji huenda akatua London ili kukamilisha zoezi la vipimo kabla ya kumwaga wino wa kuitumikia Palace.

Comments