Pep: Hart anaweza kuondoka


Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola amesema kuwa Kipa wa timu hiyo Joe Hart anaweza kuondoka kama hana furaha kwenye timu hiyo.

Hart ambaye alikosa mechi dhidi ya Sunderland na ile ya Bucuresti aliweka wazi kuwa amechoshwa na hali ya kuwekwa benchi na kocha huyo.

"Huwa sipendi mchezaji akose furaha kwenye timu, ikiwa anataka kuondoka bila shaka anaweza kwenda." Alisema Pep

"Ikiwa ataamua kubaki itakuwa ni faida kubwa kwake nadhani ana nafasi kubwa ya kurejesha kiwango chake na kuimarika chini yangu." Aliongeza Pep

Endapo kipa huyo atachukua uamuzi wa kuondoka kwenye timu hiyo itakuwa shangwe kwa Sevilla na Borrusia Dortmund ambao wanahitaji huduma ya kipa huyo mwenye miaka 29 kwa sasa.

Comments