Manchester united imekamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba kwa dau la £89 kama ada ya uhamisho.
Pogba 23, alikamilisha zoezi la vipimo na kusaini mkataba wa miaka mitano ambao unamwezesha kupokea mshahara wa paundi 290000 kwa wiki.
Kwa upande wa Pogba alisema kuwa ana furaha kurejea Manchester united kwa mara nyingine na kuhaidi kufanya mambo makubwa kwenye timu hiyo.
"Nina furaha kurudi tena Manchester united, hii ni timu kubwa ni jambo la furaha kurejea hapa kwa mara nyingine." Alisema Pogba.
Pogba aliondoka Manchester united miaka minne iliyopita na sasa amerejea Old
Trafford kama mfalme.

Comments
Post a Comment