Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage amemtaka mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hans Poppe kumwomba radhi ndani ya siku 3.
Hans alimtuhumu Rage kuwa alihamishia pesa za usajili wa Mbwana Samatta kwenye akaunti ya mkewe jambo ambalo limepingwa vikali na kiongozi huyo wa zamani wa Simba.
"Jambo hili nimelifikisha kwa wakili wangu namtaka Hans Poppe aniombe msamaha ndani ya siku 3 vinginevyo suala hili litafika mahakamani." Alisema Rage
Suala la rais wa Simba Evans Aveva kushikiliwa na takukuru kuhusiana na fedha za usajili wa Okwi ndiyo umezua mzozo huu kusababisha viongozi hao kupigana vijembe.
Comments
Post a Comment