Kocha wa Leicester city Claudio Ranieri amesaini mkataba wa minne kuendelea kuinoa timu hiyo hadi 2020.
Baada ya kusaini mkataba huo kocha huyo alisema kuwa bado ataendelea kuhamasisha hali ya kujituma na kupiga kazi uwanjani katika mechi zote.
"Bado tutaendelea kupambana, msimu uliopita tulipambana na kujituma na tukaweza kuleta maajabu kwenye soka." Alisema Ranieri
Kocha huyo ambaye amefundisha timu kadhaa barani Ulaya 2015/16 ulikuwa msimu wake wa kwanza kunyanyua kombe la ligi kuu tangu alipoanza kuwa kocha.

Comments
Post a Comment