Mshambuliaji na nahodha wa Simba Mussa Hassan Mgosi amestaafu rasmi soka baada ya kuagwa kwenye uwanja wa taifa leo.
Simba inacheza mchezo wa kirafiki na URA ya Uganda ambapo nahodha huyo alicheza kwa dakika 4 kama sehemu ya kuaga rasmi soka la ushindani.
Mgosi ambaye alikabidhi cheo chake cha unahodha kwa Jonas Mkude ndiye kwa sasa ndiye meneja wa klabu Simba na huenda tukamuona katika suti kwenye mechi mbali za timu hiyo.
Mgosi alitua Simba mwaka 2005 akitokea mtibwa ambapo alidumu kwa miaka 6 na kurudi tena Mtibwa hata hivyo mwaka jana alirejea tena Simba kumalizia mpira wake.

Comments
Post a Comment