Mshambuliaji nyota Duniani Christiano Ronaldo amepata nafuu ya majeraha yake na sasa amerejea mazoezini.
Ronaldo ameanza mazoezi binafsi kama ilivyo kwa Karimu Benzema ambao wote kwa pamoja walikuwa wakisumbuliwa na goti.
Kwa upande wa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema ni habari njema kama Ronaldo amepata nafuu ili kuweza kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.
"Ni jambo jema kurejea kwa Ronaldo, na benzema yuko njiani kurejea wote wameanza mazoezi binafsi, ni wachezaji muhimu kwenye timu."Alisema Zidane

Comments
Post a Comment