Nahodha wa Ureno Christiano Ronaldo ndiye mchezaji bora barani Ulaya msimu 2015/16 baada ya kuwazidi Lionel Messi pamoja na Luis Suarez.
Ronaldo alipata kura nyingi zaidi ambazo zilipigwa na wajumbe 55 wa kamati maalum ya UEFA ambao ni waandishi wa habari na kuweza kuibuka kifua mbele dhidi ya washambuliaji hao wa Barcelona.
Licha ya kukosa kombe la Premiera La liga, Ronaldo maarufu kama CR7 aliingoza Real Madrid kutwaa komba la mabingwa barani Ulaya, pia Ureno timu ya taifa ya Ureno katika michuano ya UEFA Euro nchini Ufaransa.
Licha ya kutwaa tuzo hii bado Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mwanasoka wa dunia maarufu kama Ballon d'or.

Comments
Post a Comment