Rooney ni jibu kwa Mkhitaryan


Bila shaka Henrikh Mkhitaryan ni mchezaji mzuri uwanjani, hakuna utata juu ya hilo, dunia yake ya soka ikijulikana zaidi baada ya kusajiliwa na Jurgen Klopp wakati kocha huyo alipokuwa Borrusia Dortmund.

Kwa umaarufu wake ilikuwa rahisi kufikiria huenda nyota huyu wa Uturuki angeingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester united lakini haikuwa rahisi kama wengi walivyodhani.

Jose Mourinho anatumia mfumo 4-2-3-1, mfumo ambao unabeba umaarufu mkubwa duniani dunia unatumiwa ata na baadhi ya timu England ikiwemo West Ham chini ya Slaven Bilic.

Ukitoa beki line ya Manchester united bila shaka pea ya viungo wawili Manchester united ni Paul Pogba pamoja Mouraine Fellaini, nadhani kuna Juan Mata upande wa kulia akicheza kama wingi midfielder, lakini yupo Antony Martial kushoto, apa ndani anapatikana Wayne Rooney akicheza nyuma ya Strika ambaye ni Zlatan Ibrahimovic.

Mkhitaryan ni fundi wa mpira, ila jina la Wayne Rooney ni kubwa kuliko ujuzi wake pale Manchester united, ni mchezaji anayependwa na mashabiki kutokana na mambo makubwa aliyofanya wakati wote akiwa na Manchester united.

Mourinho anajua namna ya kucheza ha mashabiki, anajua wanawaza nini kwenye vichwa vyao na ndiyo maana nafasi ya Mkhitaryan imekaliwa kwenye kapeti.
Fellaini na Pogba bila shaka wao ndiyo chaguo namba moja kwenye eneo la kiungo. 

Katika nafasi zao Fellaini na Pogba Mkhitaryan si mzuri kucheza namba 6 au 8, yeye ni kiungo mshambuliaji anayetakiwa kuendesha timu.

Mkhitaryan si mzuri akitokea pembeni kama Juan Mata. Mata alizoea maisha yale tangu akiwa Valencia hakuna jambo la ajabu kushangaa Juan Mata akicheza ndani na pembeni nadhani kwa Mkhitaryan ni tofauti na ndiyo maana anatokea benchi akiwa miongoni mwa wachezaji wa akiba.

Hakuna ubishi Wayne Rooney ndiye kikwazo kwa Mkhitaryan, iwapo Wayne ambaye ni nahodha wa England na Manchester united atapata majeraha ya muda mrefu basi bila shaka Mkhitaryan atapata nafasi kikosi cha kwanza.

Haya ni mambo ambayo yapo kwenye soka haijatokea kwa Mkhitaryan, pia James Rodriquez wa Real Madrid anasugua benchi si kwamba ni mchezaji mbaya bali amekutana na watu ambao ni wafalme pale Bernabeu, akiwemo christiano Ronaldo, pamoja na Gareth Bale.

Comments