Mshambuliaji wa Taifa Stars Mbwana Samatta anazidi kuinua jina lake kwenye timu ya Genk baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa bao 2-0 dhidi ya NK Lokomotiva.
Samatta alifunga bao hilo dakika ya kwanza ya mchezo, huku lile la pili likiwekwa nyavuni na Leon Bailey.
Kwa matokeo hayo kunaifanya Genk kusonga mbele kutokana na idadi ya mabao 4-2, ikijumishwa na matokeo ya mechi ya awali ambao timu hizo zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 2-2.
Katika sare ya kwanza dhidi ya NK Lokomotiva, Genk ikiwa ugenini Samatta alizamisha nyavuni bao zote mbili mbili kabla ya Lokomotiva kuchomoa na kuyafanya matokeo kuwa 2-2.

Comments
Post a Comment