Nahodha wa Taifa Stars mbwana Samatta azidi kung'ara baada ya kutupia nyavuni bao la pili jana katika michuano ya Europa ligi.
Genk ikiwa ugenini ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya NK Lokomotiva ambao walichomoa bao zote kipindi cha pili.
Samatta alikamilisha idadi ya mabao mawili kwa timu yake baada ya kufunga kwenye dakika ya 47 bao ambalo Genk waliamini wamemaliza mechi.
Hata hivyo Lokomotiva walikuja kasi na kuchomoa bao zote mbili ambazo Genk ilitangulia kuzipata na kuyafanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mechi.

Comments
Post a Comment