Samatta azidi kuwa tishio Ubelgiji


Mbwana Samatta amezidi kuonesha thamani yake katika timu ya Genk baada ya kutupia goli nyavuni goli 2 dhidi ya Lokelen.

Samatta alifunga bao la kwanza dakika 34 na kutupia nyavuni bao la pili dakika ya 38 ambapo mshambuliaji mwenzake Leon alifunga bao la mwisho dakika ya 90 na kukamilisha idadi ya mabao 3-0.

Samatta anazidi kuwa bora na kuionesha dunia ya soka alistahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika huku akiendelea kutikisa kwenye hatua ya kufuzu Europa ligi.

Nahodha wa taifa stars ameanza kuteka hisia za mshabiki wa Genk na huenda akafungua milango ya kusonga mbele zaidi kwenye ligi kubwa duniani.

Comments