Kiungo wa timu ya Manchester United, Bastian Schweinsteiger ambaye alitangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani mwezi july leo atacheza mechi yake ya mwisho kwa timu hiyo ya Ujerumani dhidi ya Finland.
Schweinsteiger (31) ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi wakiwa na kikosi cha Ujerumani, akiwa amecheza mechi 120 na kufunga goli 24 na alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Ujerumani kilichoshiriki Euro 2016 akicheza mechi tano kabla ya kutolewa na mwenyeji Ufaransa katika nusu Fainali.
Schweinsteiger aliyeanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2004 amestaafu akiwa amechukua kombe la dunia 2014 baada ya kumfunga Argentina katika fainali iliyochezwa nchini Brazil.

Comments
Post a Comment