Kiungo wa Ujermani Bastian Schweinsteiger amesema kuwa hana mpango wa kucheza kwenye klabu nyingine barani Ulaya zaidi ya Manchester united.
Licha ya kuwa mchezaji huyo si chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho lakini Mjermani huyo amesema hana sababu ya kucheza timu nyingine barani Ulaya.
"Naheshimu timu zote, nadhani nilikuja Manchester united kwa sababu ndiyo tu pekee iliyonivutia nadhan sina haja ya kucheza kwenye timu zingine." Alisema Schweinsteiger
"Nitakua tayari kucheza nikihitajika kwenye timu. Nawashukuru kwa mchango na furaha yao ambayo imeshangaza kwa wiki chache zilizopita." Aliongeza Schweinsteiger
Schweinster amekuwa kwenye wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa Henrikh Mkhitaryan pamoja na Paul Pogba.

Comments
Post a Comment