Simba yafanya balaa taifa, wang'arisha siku yao


Simba imeanza kurejesha imani kwa wanachama na mashabiki wake baada ya kuitwanga FC Leopard ya Kenya mabao 4-0.

Simba ilicheza kwenye kiwango cha hali ya juu kipindi chote cha dakika 90 huku wachezaji wote walionza na walioingia kipindi cha pili wakionesha kandanda safi.

Simba ilipata magoli kupitia Ibrahim Ajib aliyefunga mawili, Shiza kichuya pamoja na mshambuliaji Laudit Mavungo aliyefunga bao la nne.

Mavugo, Bokungu, na wachezaji wote waliosajiliwa kutoka Mtibwa akiwemo Yasin Muzamir, Shiza Kichuya na Mohamed Ibrahim walionesha thamani yao baada ya kucheza kwenye kiwango cha hali ya juu.

Comments