Simba inadai nini kwa Hassan kessy?


Jana kamati ya hadhi na sheria ya wachezaji iliweka wazi kuwa Hassan Kessy yupo huru kuendelea kuitumikia timu yake ya sasa wakati ikipitisha usajili wa wachezaji ligi kuu.

TFF ilithibisha kuwa mkataba wa Kessy na Simba ulifikia kikomo Juni 25 mwaka huu, na beki huyo aliyechipukia mtibwa sugar alikuwa huru kusajiliwa na timu nyingine.

Haji Manara ambaye ni Afisa habari wa timu ya Simba alithubutu kusema endapo hawataweka kamati itakayosikiliza madai yao wataidhinisha vurugu na maandamano.

Nilitegemea kumsikia Haji Manara kuzungumzia ni vipi wana mkataba na Kessy na ikiwa TFF kupitia msemaji wake Alfred Lucas waliweka wazi endapo wana madai binafsi baina ya wao na Kessy au Yanga wangemalizana wenyewe.

Dunia ya sasa imetawaliwa na ukweli na uwazi, kwenye siasa na soka nadhani Uongozi wa Simba unatakiwa kuweka wazi madai au mkataba ulio hai kuonesha Kessy alivunja makubaliano.

Nadhani njia za busara zinaweza kutumika kuliko kupiga kelele zisizo na msingi na kuongeza chuki zisizo na sababu kwa mashabiki na wapenzi wa soka.

Comments