Timu ya Simba inapata nafasi kwa mara nyingine kuwaonesha mashabiki wake uimara wa timu hiyo siku ya jumapili itakaposhuka dimbani dhidi ya URA ya Uganda.
Azam iliomba kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya URA ambapo siku ya ijumaa mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Azam pale Chamanzi.
Simba imeamua kutumia nafasi hiyo na ili kupima nguvu kikosi chake kwa mara nyingine kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2016/17.
Katika mchezo wa mwisho uliochezwa siku ya Simba day, timu hiyo ilionesha cheche zake za awali baada ya kuifunga AFC Leopard ya Kenya bao 4-0.

Comments
Post a Comment