Simba yaifata Serikali ya Magufuli Dodoma


Timu ya Simba itaondoka kesho kuelekea Dodoma ambapo Septemba 3 mwaka huu timu hiyo itacheza mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Simba kupitia msemaji wake Haji Manara hatua hiyo ni sehemu ya kuisapoti serikali katika kujitahada zake za kuhamia Dodoma.

Manara alisema kuwa siku ya jumamosi wataandaa bango maalum ambalo litabeba ujumbe utaobeba dhamira hiyo ya Serikali.

"Tutaondoka siku ya alhamisi kuelekea Dodoma na Septemba 3 tutacheza mechi kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma." Alisema Manara

"Hatua hiyo ni sehemu ya kuisapoti serikali katika mpango wake wa kuhamisha serikali mkoani hapo, tutakuwa na bango kubwa kwa ajili uhamasishaji huo." Aliongeza Manara.

Comments