Timu ya Simba imeanza vizuri ligi kuu baada ya kuichapa Ndanda ya Mtwara mabao 3-1.
Simba ilipata mabao hayo kupitia Laudit Mavungo aliyeunganisha mpira wa adhabu, huku mengine mawili yakifungwa na Fredrick Blagnon pamoja na Shiza kichuya huku lile la Ndanda likiwekwa nyavuni na Juma Mponda.
Simba inaonekana kuimarika zaidi sehemu ya kiungo ambapo nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude na Mzamiru Yasini walimudu vema eneo hilo.
Katika mechi nyingine Stand ikiwa nyumbunyumbani ilishindwa kutamba mbele ya Mbao FC ambayo imepanda daraja msimu na hadi mwisho wa mpira timu hizo hazikufangana.

Comments
Post a Comment