Simba, Yanga kumfuata Azam Chamanzi


Kilio cha timu ya Azam kimeanza kusikika kuhusiana na suala la kutumia uwanja wake katika mechi za Simba na Yanga ambapo timu hizo kubwa zitaanza kufanya hivyo muda wowote kuanzia sasa.

Kwa upande wa klabu ya Yanga wao wameridhia suala hilo ingawa kulikuwa na ugumu kidogo katika timu ya Simba lakini kulinga mkurugenzi mtendaji wa timu ya Azam Saadi Kawemba mambo yanakwenda vizuri kwa sasa.

Simba ambayo inakutana na Azam katika raundi ya tano ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu itakuwa mgeni wa Azam katika uwanja katika Uwanja wa Chamanzi Complex ikiwa ni hatua za mwanzo kwa timu ya Azam kutumia uwanja huo kwa mechi za Simba na Yanga.

Kulingana na kanuni za FIFA pamoja CAF timu ya Azam ina haki zote za kutumia uwanja huo kwa kuwa umeanza kutumika katika mechi za kimataifa.

Comments