Uongozi wa Simba kupitia msemaji wa klabu Haji Manara wametoa shukrani kwa wanachama na mashabiki wa Simba waliohudhuria kwenye maadhimisho ya timu hiyo jana.
Jana Simba ilitimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1936, ambapo sherehe hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama na mashabiki wake.
Simba ilikuwa na matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo ikiwemo kutambulisha uzi mpya wa timu hiyo, wachezaji wapya na kuwaonesha mashabiki kikosi chao kilivyo imara kwa kumenyana AFC Leopard kutoka Kenya.

Comments
Post a Comment