Timu ya taifa ya England itakutana na Spain katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa November 15 mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley.
England iko chini ya Sam Alladyce ambaye ndiye mrithi wa Roy Hogdson anataka kutumia nafasi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na mechi za kufuzu kombe la dunia 2018.
Pia mechi hiyo ina faida kwa kocha mpya wa Spain Julen Lopetegui ambaye ndiye mrithi wa kiti cha Vicent del Bosque kupima kikosi chake kuelekea Russia 2018.
Spain ina kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 ukiwa ni ushindi mnono iliyowahi kupata ilipomenyana na England pale Wembley.

Comments
Post a Comment