Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ameonesha yeye ni nouma baada kufunga bao 3 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Hispani Barcelona ikishinda 6-2 dhidi ya Real Betis.
Mbali na Luis Suarez pia nyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga magoli mawili na bao lingine liliwekwa nyavuni na Arda Turan.
Suarez ambaye alikuwa mfungaji bora msimu uliopita, amefungua ukurasa wa mabao na sasa anasimama kileleni akifuatiwa na Ruben Castro na Lionel Messi ambao wote wamefunga mara 2.

Comments
Post a Comment