Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimbani Septemba 3 badala ya tarehe 2 kama ilivyopangwa dhidi ya Super Eagles.
Kocha wa timu ya taifa Bonifasi Mkwasa anatarajia kuita kikosi chake kitakachopaa
nchini Nigeria katika mchezo wa marudiano.
Kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa nyumbani Stars ilitoka sare na isiyokuwa na magoli baada ya kutoshana nguvu na Super Eagles ambao haukushirikisha baadhi ya nyota wao wanaocheza ligi kubwa barani Ulaya.

Comments
Post a Comment