Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji imepitsha usajili wa timu za ligi kuu ikiwemo jina la mchezaji Hassan Kessy ambaye usajili umekuwa na utata.
Kwa mujibu wa Alfred Lucas ambaye ni afisa habari wa TFF amethibisha kuwa sasa mchezaji huyo hana kipingamizi cha kutumika kwenye timu yake.
Juzi katika mechi ya ngao ya hisani Kessy aliingia uwanjani kuitumikia Yanga kwa mara ya kwanza jambo ambalo lililamikiwa na wadau wa Simba na Azam ambao wanafahamu usajili wa mchezaji huyo haukukamilika.
TFF imemaliza utata kuhusiana na Kessy na sasa ni jambo la neema kwa Yanga ambao watakuwa huru kumtumia nyota huyo.

Comments
Post a Comment