Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imetoa onyo kutumika kwa wachezaji watano ligi kuu baada ya kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji kutoridhishwa na usajili wao.
Majimaji
Mchezaji George Pole ambaye kwa sasa amesajiliwa na Majimaji hataruhusiwa kucheza kutokana na adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja alipokuwa kimondo FC na huku akibainika kubadili jina kimakosa na kutumia jina la Gerald Pole angali ni mchezaji yule yule.
Mwadui
Mchezaji William Lucia maarufu kama Gallas amefungiwa mwaka mmoja na TFF baada ya kusaini Mwadui angali ana mkataba wa mwaka mmoja na Ndanda.
Mbeya
Said Mkopi anazuiliwa kucheza ligi kuu kutokana na kusajili timu mbili tofauti hivyo TFF imezuia ushiriki wake ligi kuu.
African Lyon
Mchezaji Rehan kibingu amezuiliwa kucheza ligi kuu na TFF mpaka timu hiyo itakapomalizana na Ashanti Agosti 27 mwaka huu.
Mbao FC
Mchezaji Emanuel Kichiba anazuiliwa pia kusakata kabumbu ligi hadi timu hiyo itakapomalizana na Ashanti agosti 27 mwaka huu.
Mchezaji Emanuel Kichiba anazuiliwa pia kusakata kabumbu ligi hadi timu hiyo itakapomalizana na Ashanti agosti 27 mwaka huu.

Comments
Post a Comment