Timu ya taifa ya Uganda maarufu kama The Cranes watashuka dimbani leo katika mechi ya kujipima nguvu dhdi ya Kenya 'Harambee Stars' ambayo inachezwa nchini Uganda.
Uganda ipo kwenye mkakati wa kujiandaa kuikabili Comoro ambapo katika mechi hiyo anahitaji ushindi au sare kufuzu kuelekea kwenye michauno ya kombe la mataifa Africa (AFCON) itakayofanyika nchini Gaboni mwaka 2017.
Kwenye mechi hiyo pia atakuwepo kiungo wa Tottenham Hotspurs Victor Wanyama ambaye ameshawasili kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa majira ya saa kumi za jioni.

Comments
Post a Comment