US Open Vigogo Watesa


Muingereza aliyeibuka na medali ya dhahabu katika michezo ya Olympiki Andy Murray, ameendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Us Open raundi ya Kwanza baada ya kumshinda Lukas Rosol kutoka Jamhuri ya Czech kwa seti 6-3,6-2,6-2.
katika raundi ya pili ya michuano hiyo Murray atacheza dhidi ya Mhispania marcel Granollers.
Wakati huo huo katika US open, mcheza tenis namba moja kwa ubora upande wa wanawake  Serena Williams ameshinda raundi ya kwanza dhidi ya Mrusi Ekaterina Makarova kwa seti 6-3,6-3 na kufanikiwa kuingia raundi ya pili.

Comments