Usajili wa maji wa jioni EPL, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili


Sliman Islam ametua Leicester city akitokea Sporting Lisbon ya Ureno kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekw wazi.

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ametua kwa mkopo wa mwaka mmoja katika timu ya AFC Bournemouth.

Beki wa Real Madrid  Alvaro Arbeloa amejiunga na timu ya West Ham kwa muda wa mwaka moja, mchezaji huyo ametua bure kwenye timu hiyo.

David Luis amerejea tena Chelsea baada ya PSG kumwachia mchezaji huyo kwa dau la £30 milioni ambalo timu hiyo imeridhia kutoa.

Moussa Sissoko kutoka Newcastle ametua Tottenham na kusaini mkataba wa miaka 5 ya kutumikia timu hiyo.

Comments