Usikkose mchezo wa ngao ya Hisani kati ya Manchester united v Leicester city


Mshambuliaji wa Leicester city Jamie Vardy yuko fiti kucheza mchezo wa leo dhidi ya Machester united katika dimba la Wembley.

Bila kusahau uwepo wa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambaye usajili wake umeleta  mvuto wa aina yake katika timu ya Manchester united atakuwepo katika dimba la Wembley leo.

Licha ya kupoteza mechi dhidi ya Borrusia Dortmund ambayo walishinda magoli 4-1 Mourinho anaamini kuna ushindi kwa timu yake leo.

Kwa upande wa Ranieri anasema amesahau yaliyopita na sasa anafikiria msimu mpya wa ligi, licha ya ugumu wa mechi aliyonayo leo kocha amesisitiza kuwa watacheza kwa ajili ya ushindi, Ranieri aliongeza hakuna mechi ya kirafiki ila ni ushindani wa hali ya juu.

Pia Leicester city wana rekodi ya kupata ubingwa wa kombe la ligi katika uwanja wa Wembley baada ya kuifunga Tranmere magoli 2-1 hiyo ilikuwa mwaka 2000.

Comments